Local Bulletins

KNUT Marsabit yakanusha madai ya walimu kunyimwa huduma za matibabu kutokana na kucheleweshwa kwa fedha na TSC

Na Joseph Muchai,

Muda mfupi baada ya muungano wa hospitali za kibinafsi nchini RUPHA kutoa lalama zao kuhusiana na kucheleweshwa kwa malipo ya matibabu kutoka kwa tume ya huduma ya walimu nchi TSC sasa walimu kwenye kaunti ya Marsabit wametoa kauli yao.

Akiongea na idhaa hii katibu mkuu wa chama chama cha walimu KNUT tawi la Marsabit Rosemary Talaso amedhibitisha kuwa kumekuwa na ucheleweshaji wa malipo hayo ila akasema kuwa kwa sasa walimu katika kaunti ya Marsabit hawajakumbwa na changamoto hiyo kama maeneo mengine nchini.

Hapo awali ripoti iliyotolewa ilionyesha kuwa tume ya kitaifa ya huduma za walimu nchini TSC, tume ya kitaifa ya huduma za polisi NPS na tume ya huduma za polisi wa jela KPS zimechelewa kulipa fedha hitajika kwa shughuli za matibabu.

Aidha ripoti hiyo ilionyesha kuwa walimu 452,635 nchini wameadhirika kutokana na kucheleweshwa kwa fedha hizo.

Subscribe to eNewsletter