Wazee waonywa dhidi ya kusuluhisha kesi za dhulma za kijinsia vijini…
January 30, 2025
Na Joseph Muchai,
Huku ongezeko katika maambukizi ya ugonjwa wa malaria likizidi kushuhudiwa katika kaunti ya Marsabit serikali ya kaunti kipitia wizara ya afya imesema kwamba iko tayari kukabiliana na magonjwa yanayoambukizwa na pia yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Akiongea na kituo hiki waziri wa afya kaunti Marsabit Malicha Boru amesema kwamba uhaba wa maji umechangia pakubwa katika ongezeko hilo hata hivyo akisema kwamba serikali ya kaunti imejizatiti ili kuhakikisha kuwa wakaazi wako salama.
Aidha waziri Boru amesema kuwa wahudumu wa afya ya umma wamejitolea kukabiliana na magonjwa na pia kuhakikisha kuwa huduma zinawafikia walio mashinani.
Pia amesema kuwa vituo vipya vya afya vinaendelea kufunguliwa katika maeneo ya mashinanani kama njia muhimu ya kuboresha sekta ya afya jimboni.