Wazee waonywa dhidi ya kusuluhisha kesi za dhulma za kijinsia vijini…
January 30, 2025
Na Samuel Kosgei
SERIKALI ya kaunti ya Marsabit inalenga kuendeleza zoezi la kupunguza idadi ya wafanyakazi katika idara mbali mbali za kaunti.
Katibu wa kaunti na pia mkuu wa wafanyakazi wa kaunti Hussein Sasura ameambia shajara kuwa lengo kuu la zoezi hilo ni kupunguza gharama ya kulipia mishahara ya wafanyakazi ambayo ni zaidi ya nusu ya bajeti nzima ya kaunti.
Kulingana naye ni kuwa mwaka jana wafanyakazi 120 ambao kandarasi zao zilikamilika waliondoka baada ya kukosa kuongezewa kandarasi nyingine, wafanyakazi vibarua 160 walifutwa mwezi wa 10 na zaidi ya watu sitini waliofikisha miaka 60 pia wakiondoka.
Kwenye barua kwa idara mbalimbali za kaunti wiki jana, Sasura alisema kuwa wafanyakazi vibarua watapunguzwa kwa asilimia 50. Kurefushwa kwa kandarasi kulisitishwa na kupandisha watu madaraka kumesimamishwa kwa sasa pia.
Hatua hiyo anasema inalenga kupunguza gharama ya kulipa wafanyakazi baada ya mgao wa kaunti kupunguzwa na serikali kuu.
Kwenye kongamano la kitaifa la kuangazia gharama ya kulipa mishahara za kaunti zote nchini mwezi juni mwaka jana serikali kuu iliagiza kaunti kutathmini upya malipo ya mishahara iliyotajwa kuwa kubwa sana huku pesa za maendeleo zikupugua.