Wazee waonywa dhidi ya kusuluhisha kesi za dhulma za kijinsia vijini…
January 30, 2025
Na Waandishi Wetu,
Mwanaume mmoja ameshtakiwa katika mahakama kuu ya Marsabit kwa mauaji.
Mahakama imearifiwa kuwa mnamo tarehe kumi na tatu mwezi Oktoba mwaka wa 2023 katika eneo la Diibu Dadacha kaunti ndogo ya Sololo, kaunti ya Marsabit mshukiwa Doti Waqo Sora alimuua mamake Safao Waqo kwa kumkatakata.
Mshukiwa aliwasilishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tarehe 8 mwezi Januari mwaka wa 2024 mbele ya aliyekuwa jaji wa mahakama kuu ya Marsabit Jessy Nyagah.
Tarehe 10 Aprili 2024 mahakama kuu iliagiza mshukiwa kufanyiwa uchunguzi wa afya ya akili katika hospitali ya Mathare jijini Nairobi.
Mnamo tarehe 31 mwezi julai mwaka 2024 mahakama ilielezwa kuwa mshukiwa alipelekwa hospitalini kwa uchunguzi na kubaina kuwa yuko sawa kufunguliwa mashtaka.
Hakimu wa mahakama kuu ya Marsabit Francis Olel ameagiza mshukiwa kusomewa upya mashtaka tarehe5 mwezi Februari mwaka huu wa 2025.