Local Bulletins

Zaidi ya wanafunzi 500 katika shule saba za upili, eneo bunge la Laisamis wanufaika na mradi wa Food for Fees kutoka shirika la Kenya Drylands Education Fund (KDEF).

Na Isaac Waihenya,

Zaidi ya wanafunzi 500 katika shule saba za upili katika eneo bunge la Laisamis wamenufaika na mradi wa kuwalipia karo kupita chakula, maarufu Food for Fees kutoka kwa shirika lisilo la kiserekali la Kenya Drylands Education Fund (KDEF).

Akizungumza wakati wa zoezi la uzinduzi wa mradi huo mwaka huu wa 2025, lililoandaliwa katika shule ya upili ya Karare Mixed,mkurugenzi mkuu wa shirika la KDEF nchini Ahmed Kura amesema kuwa mradi huo unalenga kupunguza mzingo wa karo haswa kwa wanafunzi wanaotoka katika familia zenye kipato cha chini.

Katika mpango huo shule hizo saba zilinufaika na bidhaa muhimu za matumizi kama vile, mahindi maharagwe, sukari, mchele, mafuta ya kupika pamoja na chumvi.

Shule ya Merrille mixed ilipata magunia 35 ya mahindi na magunia 20 ya maharagwe, Karare Mixed ikipata magunia 25 ya mahindi na 15 ya maharagwe, shule ya upili ya Korr ikipata magunia 26 ya mahindi na magunia 8 ya maharagwe, ile ya Illaut ikipata magunia 15 ya mahindi na magunia 5 ya maharagwe, nayo shule ya upili ya Log Logo girls ikipata magunia 26 ya mahindi na magunia 8 ya maharagwe huku shule ya upili ya Tirrim ikipata 26 ya mahindi sawa na magunia 8 ya maharagwe.

Aidha Kura amesema kuwa wanalenga kupanua mradi huo hadi katika maeneo bunge ya Saku na Northhorr katika siku za usoni.

Vile vile mkurugenzi mkuu huyo wa shirika la KDEF amewataka viongozi wa jimbo hili kushirikiana ili kupiga jeki kiwango cha elimu katika kaunti ya Marsabit.

Hata hivyo baadhi ya wanafunzi walionufaika na mradi huo wa Food for Fees katika shule ya upili ya Karere Mixed wakiongozwa na Joan Letoimanga wamelishukuru shirika la KDEF kwa kuhakikisha kwamba wanapata elimu bora kama wanafunzi wengine kutoka sehemu zingine za nchi.

Subscribe to eNewsletter