Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
Na Waandishi Wetu.
Mwanamke mmoja na wazazi wa mume wake wamekamatwa na maafisa maafisa wa polisi katika eneo la Dololo Boji kaunti ndogo ya Dukana kaunti ya Marsabit baada ya kudaiwa kushirikiana kuwaua watoto mapacha waliozaliwa siku ya Jumapili.
Kamishna msaidizi wa divesheni ya Dukana Nazarene Njuki amedai kuwa watoto hao mapacha waliuliwa na wazazi wao pindi tu walipofika nyumbani baada ya kutoka hospitali, hii ni kutokana na Imani ya kitamaduni kuwa watoto wa kwanza mapacha katika jamii ya Gabra ni “ishara ya laana kwa familia.”
ACC Njuki anasema kuwa chifu wa eneo hilo ndiye aliyeripotiwa kuuawa kwa watoto hao na kuzikwa kijijini hapo kwa siri nyakati za usiku.
Amesema kuwa kulingana na daktari wa kituo cha afya cha Dukana ni kuwa watoto hao walikuwa wazima kabisa walipopewa wazazi wake. Walisindikizwa nyumbani na ambulensi hadi kwao baada ya mama yake Umuro Isacko kupata nguvu.
“Wakati chifu alipata habari kuwa watoto mapacha wamezaliwa kuna uwezekano wale watoto kudhulumiwa au kuuawa… chifu, mdogo wake na askari kufika eneo la Dolo Boji, wakakuta ni kweli watoto waliuliwa na kuzikwa ndani ya nyumba…” alisema kamishna msaidizi.
Njuki amesema kuwa mauaji ya watoto hao imesababishwa na mila potovu iliyopitwa na wakati. Kulingana na DO Njuki ni kuwa huenda watoto hao wawili msichana na mvulana waliuliwa kwa kunyimwa hewa kulingana na maelezo ya chifu.
“Kulingana na mila na desturi ya jamii ya Gabra kitambo kulikuwa na mafikira kuwa ukipata mapacha kama watoto wa kwanza wataleta bahati mbaya na kusababisha maafa au mambo mabaya” akasema ACC Njuki.
Njuki amekemea na kuonya kuwa ni kinyume cha sheria kuua binadamu yeyote bila kujali utamaduni na mila za jamii yoyote nchini. Amelaumu pia wanakijiji kwa kunyamazia uovu wa kitamaduni kufanyika bila wao kuripotiwa kwa idara za serikali kwa wakati.
“Ni hatia kubwa kuua kwani wanakijiji wananyamazia vitendo hivyo kwani hawaoni ajabu au ubaya wowote ndiposa wanasema hawakuona chochote au kuskia kaburi likichimbwa usiku” alikariri ACC Njuki.