Local Bulletins

Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.

Na JB Nateleng

“Matamshi ya rais mstaafu uhuru Kenyatta, kuhusu kupigania haki yanatia motisha wakenya na kuwapa nguvu ya kuendelea mbele”

Hii ni kauli yake Harrison Mugo ambaye ni mwekahazina wa chama cha kisiasa cha National Vision Party (NVP).

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee Mugo amesema kuwa ni wakati muhimu kwa wakenya kuweza kuamka na kutetea haki yao na kuwawajibisha viongozi ambao wamezembea kazini.

Mugo amewataka vijana wa Gen Z kuweza kumakinika na kile wanasiasa wanasema kwa kuchukua tahadhari.

Mugo amesifia umoja wa vijana wa Kenya na kuwataka kuzidi kuungana ili kuleta mabadiliko nchini kwa kufuata sheria na kuwashinikiza viongozi kufanya kazi ipasavyo huku akiwataka kuwa macho hadi wakati wa uchaguzi wa 2027 ili kuwang`atua mamlakani viongozi ambao hawakuendeleza ajenda ya maendeleo.

Kuhusiana na suala la IEBC, Mugo amesema kuwa ni sharti serekali iharakishe mchakato wa kumbuni tume huru ya uchaguzi (IEBC), ili kuruhusu wakenya kutekeleza haki yao ya kuchagua viongozi.

Mugo ameitaka serekali kuacha kuteka nyara vijana na badala yake kutimiza malengo ya kuleta maendeleo mashinani na kuwawezesha vijana.

Subscribe to eNewsletter