Local Bulletins

Wizara ya afya Marsabit yadhibitisha uhaba wa chanjo ya BCG kama ilivyo kote nchini.

Na Carol Waforo

Wizara ya afya jimboni Marsabit imedhibitisha uwepo wa uhaba wa chanjo ya BCG kama inavyoshuhudiwa  katika sehemu nyingi nchini.

Haya yamewekwa wazi na waziri wa afya jimboni Marsabit Malicha Boru ambaye amezungumza na shajara ya Radio Jangwani.

Waziri amedokeza kuwa wizara ya afya nchini imeahidi kuwa chanjo hiyo itarejesha upatikanaji wake katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Aidha Waziri anasema kuwa wameweka mikakati angalau kuhakikisha kuwa vituo vilivyo na uhaba huo vinapata chanjo ya BCG.

Chanjo ya BCG hutumika dhidi ya kifua kikuu.

Jana jumatano wizara ya afya iliwahakikishia wakenya kuwa serikali inafanya kazi kurejesha upatikanaji wa chanjo hiyo ya BCG, ambayo imekosekana kwa muda sasa.

Mkrugenzi mkuu wa afya Dr Patrick Amoth alisema kuwa mamlaka ya usambazaji wa dawa nchini KEMSA imenunua dozi milioni 2.3 za chanjo hiyo ambazo zinatarajiwa kuwasili nchini ifikapo mwishoni wa mwezi huu wa februari.

Subscribe to eNewsletter