Local Bulletins

Chama cha Kitaifa cha wafanyabiashara na viwanda kinataka serikali kuwahusisha kwenye mswada wa fedha wa 2025 kinyume na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Na Samuel Kosgei

Chama cha Kitaifa cha wafanyabiashara na viwanda (KNCCI) kimerai serikali kuu kuwahusisha kikamilifu mwaka huu wanapotayarisha mswada wa fedha wa 2025 kinyume na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Naibu mwenyekiti wa chama hicho cha wafanyabiashara tawi la Marsabit Ali Noor ameambia shajara kuwa kutohusishwa kikamilifu kwa chama cha wafanyabisha ni mojawapo ya sababu mswada wa fedha mwaka jana kutofaulu kutokana na wafanyabiashara kuachwa nje na serikali.

Noor anasema kuwa kupitia wao kuhusishwa kikamilifu, kutasaidia kwani watawakilisha maoni na malalamishi ya wafanyabiashara wa chini.

Wakati uo huo amesema kuwa biashara nyingi hapa Marsabit hazifanyi vizuri na biashara nyingi haswa maduka kulingana naye yanafungwa.

Ameitaka serikali kuanzisha sera jumuishi itakayosaidia kupunguza ushuru na bei ya bidhaa muhimu haswa mafuta ya petroli.

Bei ya mafuta hayo katika taifa jirani la Ethiopia anasema iko chini ikilinganishwa na upande wa Kenya suala analosema inaathiri biashara upande wa Kenya.

Subscribe to eNewsletter