Upungufu wa maafisa wa kuhamsisha umaa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi wachangia kudorora kwa kilimo Marsabit…
January 17, 2025
Na Isaac Waihenya,
Mila potovu na utamaduni zimetajwa kama sababu kuu za kuwakandamiza wanawake katika nafasi za ajira na uongozi haswa katika jamii za wafugaji.
Haya yamekaririwa na mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu nchini la HURIA, Yusuf Lule.
Akizungumza baada ya kuzinduliwa kwa mpango wa utekelezaji wa usalama na amani (Action Plan), Lule amesema kuwa jamii ya wafugaji imekuwa ikitumia vigezo hivyo kuwavunja moyo wanawake wanao wania nyadhfa mbalimbali za uongozi na hata masuala ya kupambana usalama na amani.
Aidha Lule ameonya wanaotumia utamaduni uliopitwa na wakati na unaowakandamiza wanawake kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Amezitaja baadhi ya mila kama zisizofaa na ambazo zinatumiwa kuwanyamazisha wanawake na kuwazuia kutofikia malengo yao.
Hata hivyo Lule amewaonya Wakenya kutotumia mila potovu kugeuza baadhi ya aya katika vitabu vitakatifu ili kukandamiza wanawake.