Aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule ya Sasura Girls Fatuma Abdi amekabidhi uongozi wa shule hiyo kwa naibu wa mwalimu mkuu Paul Mugambi.
Akizungumza baada ya ya kukabidhi Mugambi uongozi wa shule ya upili ya Sasura girls mbele ya mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri, mwalimu Fatuma ameondoa wasiwasi Kwa wazazi kuwa alihamishwa kwa lazima akisema kuwa lilikuwa ni ombi lake la kutaka kuondoka ili kuwa karibu na familia yake.
Mkurungezi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri aliyezuru shule hiyo hii leo amesema kuwa idara ya elimu itashirikiana na tume ya kuajiri walimu (TSC) pamoja na bodi ya shule hiyo ili kuweza kuleta mwalimu mkuu mpya.
Magiri amewataka wazazi wa shule hiyo kuwa subira na kumsaidia naibu wa shule hiyo kuboresha uongozi wa shule hiyo hadi pale ambapo watapata mwalimu mkuu mwingine.