Wazazi wa shule ya upili ya Sasura girls wamkataa mwalimu mkuu mpya aliyehamishiwa shuleni humo.
January 14, 2025
Na Isaac Waihenya,
Mkurugenzi wa tume ya kuwaajiri walimu TSC tawi la Marsabit Ali Hussein Abdi amepuzilia mbali madai ya kuhusika katika kuhamisha aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Maikona Girls hadi katika shule ya upili ya Sasura Girls.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani ofisini mwake Hussein ametaja kwamba jukumu la kuwahamisha walimu wakuu lipo mikononi mwa ofisi kuu ya TSC jijini Nairobi au ofisi ya mkurugenzi wa kanda ya Kaskazini ila sio ofisi ya mkurugenzi wa kaunti.
Hata hivyo Hussein ametaja kwamba TSC imepokea malalamishi ya wazazi ambao wamemkata mwalimu mkuu mpya huyo Bi. Madina Harme ambaye alihamishiwa shuleni humu mwanzoni mwa mwaka huu, huku akitaja kwamba serekali itayaamgazia na kuyashughulikia haraka iwezekanavyo.
Vilevile Hussein amekariri kwamba ofisi yake imejitolea kushughulikia maswala yanoyofungamana na walimu hapa jimboni ili kuhakikisha kwamba wanafunzi katika kaunti ya Marsabit wanapata elimu bora.