Local Bulletins

Serikali ya kaunti ya Marsabit yakana madai ya unyakuzi wa ardhi na kutenga jamii ya Sakuye katika harakati ya kufunguliwa kwa mgodi wa Dabel.

Na Carol Waforo

Serikali ya kaunti ya Marsabit imekana madai ya unyakuzi wa ardhi inayokaliwa na migodi ya hillo iliyoko katika lokesheni ya Dabel eneo bunge la Moyale kaunti ya Marsabit pamoja na madai ya kutenga jamii ya Sakuye katika mazungumzo ya kufunguliwa kwa migodi hiyo.

Akizungumza na wanabari siku Jumatatu msemaji wa serikali ya kaunti ya Marsabit Abduba Barille alikana madai hayo akisema kuwa jamii zote zimehusishwa ikiwemo jamii ya Sakuye inayosemekana kuibua madai hayo katika moja wa mkutano ulioandaliwa siku ya Jumapili.

Barille amesisitiza kuwa madini ni mali ya umma na kila mtu ana haki yakunufaika.

Kadhalika ameeleza kuwa jamii zote katika eneo hilo zilihusihwa kikamilifu katika ufunguzi wa migodi hiyo.

Aidha serikali ya kaunti ya Marsabit imendelea kumshtumu Gavana wa kaunti ya Isiolo Abdi Guyo kwa kuchochea jamii hiyo kutoshirikiana na serikali ya kaunti ya Marsabit katika ufunguzi wa migodi hiyo.

Katika hafla moja mwaka jana gavana wa Isiolo Abdi Guyo aliapa kutetea jamii hiyo dhidi ya kile alikitaja kama unyanyasaji.

Mwezi disemba mwaka 2024, Viongozi wa jamii zinazoishi katika eneo bunge la Moyale waliwasilisha mkataba wa maelewano ya kuendeleza shughuli katika migodi hiyo ya Dabel wakati wa kikao cha kujadili mustakabali wa kufungua migodi hiyo kilichoandaliwa katika ukumbi wa shule ya wavulana ya Moyale

Japo jamii ya Sakuye haikuridhika na mktaba huo licha ya kwamba kiongozi wao alitia saini.

Subscribe to eNewsletter