Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
Idadi ya wanafunzi walioripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula wa kwanza wa mwaka wa 2025 katika kaunti ya Marsabit haridhishi kamwe.
Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri.
Akizungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani ofisini mwake, Magiri ametaja kwamba hadi kufikia sasa idadi kubwa ya wanafunzi hawajarejea shuleni huku akiwataka wazazi kuhakikisha kwamba wanao wanaripoti shuleni jumatatu wiki ijayo.
Aidha Magiri amewarai maafisa wa utawala kushirikiana kufanikisha kampeni ya watoto kurejea shuleni kwa asilimia 100.
Kuhusiana na taarifa ya waziri wa elimu kwamba kuanzia mwaka huu kutakuwepo na mitihani ya kidato cha nne KCSE mwezi Julai na mwisho wa mwaka, Magiri alikuwa na haya ya kusema.