Local Bulletins

Idara ya Watoto Marsabit yawarai wazazi kuwarejesha wanao shuleni,muhula wa kwanza wa 2025….

Wazazi katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuhakikisha kwamba wanao wanaripoti shuleni kwa muhula wa kwanza wa mwaka wa 2025.

Kwa mijibu wa afisa wa watoto katika kaunti ya Marsabit Mukanzi Leakey ni kuwa ni haki ya kila mtoto kupata elimu huku akionya kuwa idara hiyo haitawasaza wazazi watakaokosa kuwapeleka wanao shuleni kutokana na changamoto zozote zile.

Leakey akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani ofisini mwake amewarai wazazi ambao wanachangamoto za kifedha kutembelea ofisi zao ili kupata msaada.

Leakey ameweka wazi kuwa wanashirikiana na idara ya usalama kuhakikisha kwamba watoto wanapata haki zao za kimsingi.

Aidha afisa huyo wa watoto ameonya dhidi ya wazazi kuwaficha watoto wanaoishi na ulemavu na badala yake kuhakikisha kwamba wanapata haki ya elimu.

Hali kadhalika amewataka walio kwenye ndoa kusaka suluhu la mizozo inayojiri ili isije ikaadhiri haki za watoto kwa njia moja au nyingine.

Subscribe to eNewsletter