Local Bulletins

Wazazi eneo la Laisamis,kaunti ya Marsabit waonywa dhidi ya kutowapeleka wanao shuleni.

Huku shule zikifunguliwa kwa muhula wa kwanza wa mwaka 2025 leo jumatatu, wazazi wameonywa dhidi ya kutowapeleka wanao shuleni.

Ni onyo ambalo limetolewa na Chifu wa eneo la Laisamis Agostino Supeer akisema kuwa wazazi watakao kiuka haki za watoto kupata elimu watawajibishwa kisheria.

Chifu Supeer aliyezungumza na meza ya habari ya radio Jangwani kwa njia ya simu,pia amewataka vijana jimboni kukumbatia mafunzo ya kiufundi ili kuweza kujifaidi katika siku zao za baadae.

Aidha Chifu Supeer anasema kuwa wataanza msako wa kuwasaka wanafunzi ambao hawatarejea shuleni hivi karibuni huku akidokeza kuwa usalama umeimarishwa kipindi hiki wanafunzi wanarejea shuleni

Subscribe to eNewsletter