Local Bulletins

Serekali kujenga shule katikati mwa maeneo ya North Horr na Illeret, kaunti ya Marsabit.

Serekali inapania kujenga shule katika sehemu mbazo hazina shule, kaunti ya Marsabit ili kuzuia wanafunzi kusafiri mbali kusaka elimu.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri ni kuwa idara ya elimu jimboni chini ya uongozi wake imependekeza kwa wizara ya elimu hoja ya kujengwa kwa shule katikati mwa maeneo ya North Horr na Illeret ili kuhakikisha kwamba wananchi wanaoishi katika eneo hilo wanapata elimu.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani ofisi mwake Magiri ametaja kwamba serekali itahakikisha kwamba wanafunzi ambao walikuwa wanaendelea na elimu wamerejea shuleni baada ya likizo ndefu ya mwezi Disemba kutamatika.

Kando na hilo Magiri amefichua kuwa bado mipangilio ya kuhakikisha kwamaba shule ya Elmolo ambayo sehemu yake kubwa imezama kwa maji kutokana na kufura kwa ziwa Turkana inahamishwa hadi katika eneo lingine ambalo ni salama kwa wanafunzi.

Subscribe to eNewsletter