Understanding Elavil: Uses, Benefits, and Safety
December 26, 2024
Wakimbizi wa ndani kwa ndani katika kaunti ya Marsabit wanazidi kulilia serikali na wahisani kuwasaidia ili waweze kupata msaada wa chakula na mahitaji mengine ya kimsingi.
Wakizungumza katika hafla ambapo familia 50 imepokezwa mabati 30 na kanisa la kianglikana ACK Marsabit ,Guyo Sora ambaye ni mmoja wa wakimbizi amesema kuwa wanapitia changamoto kama vile ukosefu wa chakula, ukosefu wa shule na pia kupata magonjwa yanayotokana na baridi.
Askofu wa kanisa la ACK dayosisi ya Marsabit Daniel Wario Qampicha amesema kuwa wakimbizi hao wanazidi kuteseka na wamesahaulika katika jamii akisema vita vimeisha na si vyema kwa wao kuzidi kuhangaika kutokana na ukosefu wa chakula na kuishi katika mazingira ambayo hayafai.
Tura Rura ambaye ni mwakilishi wadi ya North Horr ameomba serikali kuu na ile ya kaunti kuwasaidia wakimbizi kwa kuwajengea manyumba na kuwapa chakula na pia kuhimiza wakaazi kukaa kwa Amani ili kuzuia wakimbizi Zaidi.