Local Bulletins

WAVUVI LOIYANGALANI WATAKIWA KUZINGATIA USALAMA WAO MWANZO KABLA YA KUTUMIA BOTI.

Wakaazi wanaoishi karibu na Ziwa Turkana wadi ya Loiyangalani kaunti hii ya Marsabit wanazidi kutahadharishwa kujiepusha na kuvuka Ziwa kiholela bila mpangilio mwafaka ili kuepusha ajali ambazo ushuhudiwa mara nyingi msimu huu wa sherehe za krismasi.

Afisa katika idara ya uvuvi kaunti ya Marsabit Sostine Nanjali ameambia shajara kuwa kuna haja ya wavuvi kumakinika sana wanapotumia boti zao kuenda kuvua. Amewataka wazazi kulinda watoto kutoenda kuvua wakati huu ambapo ziwa limechafuka kutokana na mawambi makali.

Vile vile amewataka wamiliki wa maboti kuhakikisha kuwa boti zao ziko katika hali nzuri kabla ya kuvuka kwani usalama wa usafiri huanza na wao wenyewe. Pia wametakiwa kuzingatia onyo na jumbe zinazotumwa kwao na idara ya uvuvi nchini.

Wanaoshi karibu na ziwa Turkana pia wametolewa wito wa kuhama kwani maji yanazidi kuongezeka kila mara suala linalohatarisha wanaoishi eneo hilo.

Wakati uo huo amewataka wavuvi kuepuka mzozo na shirika la wanyama pori nchini KWS kwa kutofika sehemu zinazolindwa haswa sehemu ambapo samaki huzalia kwani hilo husababisha kukamatwa na walinzi wa KWS.

Anasema kuwa kws ikishirikiana na idara ya uvuvi mwakani inalenga kuweka mpaka unaoonekana ili kuepusha wavuvi kufika sehemu kunakolindwa.

Subscribe to eNewsletter