Serekali yatakiwa kutoa hamasa kwa jamii kuhusiana na ongezeko la visa vya mauaji ya wanawake na wasichana nchini.
January 28, 2025
Shughuli za nyumbani pamoja na kikazi zimetajwa kama sababu kuu ya wanawake kuwa na muda mchache wa kufanya mazoezi.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Paradise club Konze Kura ni kuwa wanawake wengi hupata majukumu mengi nyumbani na hata kazini jambo ambalo linawafanya wao kukosa muda wa kufanya Mazoezi.
Konze ameelezea kuwa wanawake wengi wanaogopa kujitokeza kufanya mazoezi kwa sababu ya mila na tamaduni za hapa Marsabit ambapo mwanamke anapaswa kuomba mumewe ruhusa ama kuandamana na mumewe.
CUE IN… KONZE ON MAZOEZI.
aidha Konze amewataka akinamama pamoja na wasichana kujitokeza kwa wingi na kujiunga na wenzao ambao wanafanya Mazoezi yatayosaidia kuboresha afya zao.
CUE IN… KONZE ON WITO
Vile vile amesema kuwa kikundi cha Marsabit walk Movement kina mpango wa kuhamasisha jamii kuhusiana na utunzaji wa mazingira kwa kuwahusisha vijana katika mpango kwa usafi wa Mazingira.
CUE IN… KONZE ON MAZINGIRA