Local Bulletins

JAMII YA MARSABIT YATAKIWA KUJITOKEZA KUPIMWA UGONJWA WA MENINGITIS ILI KUPATA MATIBABU MAPEMA.

 Jamii ya Marsabit imetakiwa kujitokeza kupimwa ugonjwa wa Meningitis ili kuhakikisha kwamba wanapata matibabu mapema.

Kwa mujibu wa daktari Stive Sereti anayeshughulikia wagonjwa wanaougua maradhi hayo katika hospitali ya rufaa ya Marsabit ni kuwa ni vyema kufanyiwa vipimo vya mara kwa mara vya ugonjwa huo kwani unaadhiri hadi watoto.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani ofisi mwake Daktari Sereti amesema idadi kubwa ya watu hukosa kufika hospitali Kufanyiwa vipimo huku wakiendelea kuungua maradhi hayo kimya kimya.

Aidha Sereti ametaja dalili za ugonjwa huo kama kuumwa kwa kichwa huku akiwarai wananchi kumtembelea mtaalam wa afya iwapo watahisi maumivu ya kichwa kwa muda mrefu.

Hata hivyo daktari Sereti aameweka wazi kuwa ugonjwa wa Meningitis unatibika haswa iwapo mtu atasaka matibabu mapema.

Subscribe to eNewsletter