Local Bulletins

WAKAAZI WA MARSABIT WATAKIWA KUDUMISHA USAFI WA MIKONO ILI KUJIKINGA NA MAGONJWA

Wakaazi wa Marsabit watakiwa kudumisha usafi wa mikono ili kujikinga na magonjwa

Wito wa kudumisha usafi wa mikono ulitawala katika hafla ya kuadhimisha siku ya usafi wa mkono ulimwenguni.

Akihutubia wakazi wa kaunti ndogo ya Saku, katika zahanati ya Jirime hapa kaunti ya Marsabit, Afisa mkuu wa afya ya umma, kaunti ya Marsabit Omar Mohamed Boko amesema kuwa idara ya afya jimboni imeweza kupiga hatua katika kuhamasisha umma kuhusu usafi wa mikono pamoja na matumizi mema ya choo.

Boko ameelezea kuwa kufikia sasa ni aslimia kidogo ya wakazi ambao bado hawajapata ujumbe kuhusu usafi wa Mikono pamoja na Mazingira.

CUE IN… BOKO ON MARSABIT.

Boko alisisitiza umuhimu wa kutumia sabuni na maji safi wakati wa kunawa mikono ili kuwa na uhakika wa usafi na kukinga uchafu na magonjwa.

Kadhalika Boko amewachangamoto wakazi jimboni Marsabit kuweza kudumisha usafi wa mikono ili kujikinga na magonjwa.

 

Subscribe to eNewsletter