Local Bulletins

MILA POTOVU KAMA VILE UKEKETAJI NA NDOA ZA MAPEMA BADO ZINAREJESHA NYUMA HATUA ZILIZOPIGWA KATIKA KUINUA MTOTO MSICHANA MARSABIT.

Kuna muda wa kila kitu ila huu ni muda wenu wa masomo.

Ndio ushauri wa mtetezi wa haki za kinadamu katika kaunti ya Marsabit Nuria Golo kwa wasichana siku hii ya kusherekea siku ya mtoto msichana ulimwenguni.

Akizungumza na Radio Jangwani ofisini mwake, Nuria amewataka wasichana kutumia muda huu kujiimarisha kielimu ili kuboresha maisha yao ya baadae.

Aidha Nuria amesema kuwa japo kaunti ya Marsabit imepiga hatua kadhaa katika kuhakikisisha kuwa maisha ya mtoto msichana yameimarika ila bado kuna maswala kama vile mila potovu za ukeketaji na ndoa za mapema ambazo zinarejesha nyuma hatua zizopigwa.

Hata hivyo Nuria ametoa onyo kali kwa wale wanaoendleza dhulma za kijinsia kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Subscribe to eNewsletter