Local Bulletins

WAFANYIKAZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMETAKIWA KULIPA SWALA LA AFYA YA AKILI KIPAU MBELE WAKIWA KAZINI MWAO.

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya afya akili hii leo wafanyikazi katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kulipa swala la afya ya akili kipau mbele wakiwa kazini mwao.

Kwa mujibu wa afisa wa afya ya akili katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Victor Karani ni kuwa kuna idadi kubwa ya wafanyikazi ambao wanaadhirika na matatizo ya afya ya akili kutokana na changamoto za kikazi.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya afya ya akili yaliyoandaliwa hapa mjini Marsabit Karani amewataka wafanyikazi kutenga muda wa kupumzika na kutuliza mawazo.

Aidha Karani amewataka wasimamizi katika taasisi mbalimbali za kazi kuwapa nafasi za kupumzika ili kutuliz amawazo na kuhakikisha kwamba wanaweza kufanya kazi inavyostahili.

Kauli ya Karani imeungwa mkono na mwazilishi wa shirika linaloshughulikia maswala ya afya ya akili jimboni Marsabit la Open Mind Community Focus(OMCF) Mariam Abduba ambaye ametaja kwamba shirika hilo linalenga kuhakikisha kwamba vijana wanafunguka kuhusiiana na yale yanayowadhiri ili kuzuia maradhi ya afya akili.

Kwa upande wake kiongozi wa vijana katika eneo bunge la Saku ambaye pia ni spika wa bunge la vijana la Saku Youth Assembly(SYA)Abdiaziz Boru ameirai serekali kukaza Kamba katika kukabilia na dawa za kulevya ambazo zinaadhiri afya ya akili ya vijana.

Subscribe to eNewsletter