Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Grace Gumato
Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka saba amefariki hii leo katika eneo la Songa baada ya kuumwa na nyoka hapo jana.
Afisa mtendaji katika hospitali ya rufaa ya Marsabit Kusu Abduba amesema kuwa mtoto huyo alifikishwa katika hospitali hiyo akiwa amefariki saa za usiku.
Aidha amesema kuwa mwili huo umefanyiwa upasuaji na kudhibitishwa kuwa mtoto huyo aliumwa na nyoka.
Kusu aidha amesema kuwa hospitali ya rufaa ya Marsabit iko na dawa za kupunguza makali ya sumu hivyo amewashauri wakaazi wa Marsabit kutembelea hospitali wanapoumwa na nyoka.
Wakati uo huo Kusu pia amesema kuwa watu watatu wanauguza majeraha baada ya gari walililokuwa wakisafiria kwenda Badasa kuhusika katika ajali hiyo jana jioni.
Kusu amesema kuwa wawili tayari wameruhusiwa kuenda nyumbani na mmoja akiendelea kupata matibabu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit.
Pia amesema kuwa hospitali ya rufaa ya Marsabit inaendeleza matibabu ya bure ya macho akisema tayari watu 37 wamefanyiwa upasuaji wa macho huku watu 140 wakipata matibabu na kuruhusiwa kwenda nyumbani hiyo jana.