Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na JB Nateleng,
Ni jukumu la wananchi kuhakikisha kuwa wanapata huduma bora kutoka kwa afisi za serekali.
Haya ni kwa mujibu wa afisa kutoka Tume ya haki za Kiutawala (CAJ) almaarufu “office of ombudsman” Koech Kipkogei.
Akizungumza na idhaa hii kwenye hafla ya kutoa hamasa kwa vijana, iliyoandaliwa hapa mjini Marsabit, Koech amesema kuwa Wakenya huwa wanapata shida nyingi sana wanapoenda kutafuta huduma katika ofisi za serekali huku wengi wakilazimika kulipa ili wapate huduma.
Koech ameelezea kuwa ni sharti wananchi waripoti visa hivi kwa tume ya haki za kiutawala (CAJ) kwani wao watasaidia Katika kufuatilia na kuhakikisha kuwa haki imetendeka kwa wakenya wote.
Koech amewataka wakazi wa Marsabit kuhakikisha kuwa wamewajukumisha viongozi wote ambao wapo afisini kwa kuripoti vitendo ambavyo vinaweza kulemaza upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi.
Aidha amewarai wanaMarsabit kuasi ukabila na badala yake kuweza kuangazia maswala ya uongozi bora ambayo yataleta maendeleo katika jimbo hili na kuripoti kiongozi yeyote ambaye anashukiwa kutatiza maendeleo jimboni.
Ili kuripoti visa hivi, mwananchi anaweza akapiga simu bure kwa nambari 0800221349 ama kutuma barua pepe kwa complaint@ombudsman.go.ke.