Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Caroline Waforo
Wakaazi jimboni Marsabit wametakiwa kujiepusha na dhana potovu zinaoenezwa kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa nyani Mpox.
Haya ni kutokana na madai kuwa baadhi ya wakaazi jimboni wanawaua mbwa kwa dhana kuwa wanahusika na maambukizi ya mpox.
Tahadhari hii imetolewa na afisa anayefuatilia magonjwa jimboni Marsabit Qabale Duba.
Naye afisa wa afya katika idara ya afya Abdi Adan na ambaye ni meneja wa kituo cha kushughulikia maswala ya dharura katika kaunti ya Marsabit, amewataka wakaazi jimboni kuchukua tahadhari na kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.
Aidha wakaazi ambao wanaonyesha dalili zozote zinazoambatana na ugonjwa vya MPOX wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatembelea vituo vya afya kwa uchunguzi zaidi.