Local Bulletins

MADAKTARI MARSABIT WATISHIA KUGOMA IWAPO MALALAMISHI YAO HAYATASHUGHULIKIWA CHINI YA WIKI 2.

Na Caroline Waforo

Serikali ya kaunti ya Marsabit ina wiki mbili kuanzia leo tarehe 27 mwezi Agosti, kushughulikia matakwa yaliyoibuliwa na madaktari wa kaunti ya Marsabit.

Kwenye barua iliyotiwa sahihi na katibu wa KMPDU ukanda huu wa mashariki Dr Elvise Mwandiki madaktari watalazimika kushiriki mgomo iwapo maswala yao hayatasuluhishwa chini ya wiki mbili.

Madaktari hawa wanalalama kuchelewa kwa mshahara wa mwezi Julai kati ya maswala mengine.

Na haya yanajiri huku wizara ya afya jimboni Marsabit sasa ikisema kuwa mshahara wa mwezi julai umechelewa kutokana na kutotumwa kwa mgao wa kaunti kutoka hazina ya serikali kuu.

Akizungumza na shajara ya radio jangwani afisini mwake waziri wa afya Malicha Boru amewahakikishia madaktari kuwa fedha hizo zitalipwa.

Na huku madaktari pia wakilalama kutowasilishwa kwa makato kama vile NHIF, NSSF katika sekta mbailmbali tangia mwezi april waziri Malicha ameahidi kuchunguzwa kwa madai hayo.

Hiyo jana madaktari walitoa lalama zao huku wakitishia kushiriki mgomo iwapo matakwa yao hayataweza kuangaziwa.

Subscribe to eNewsletter