Local Bulletins

SHIRIKA LA COMPASSION MARSABIT LAWATUNUKU WANAFUNZI WALIOFANYA VYEMA KATIKA MTIHANI WA KCPE MWAKA JANA, HUKU WITO UKITOLEWA KWA WAWAZI KUWAPELEKEA WANAO SHULENI.

Na Isaac Waihenya,

Wazazi wametakiwa kuwapeleka watoto shuleni bila kuwabagua ili wapate elimu itakayowafaidi katika siku za usoni.

Haya ni kwa mujibu wa msimamizi wa shirika la Compassion tawi la Marsabit mchungaji Joseph Diba.

Akizungumza wakati wa sherehe za kuwatunuku wanafunzi waliofanya vyema katika mtihani wa kitaifa wa KCPE mwaka jana,Diba amewataka wazazi kuhakikisha kwamba Watoto wote wanapata elimu huku akiwarai kutoa ripoti kwa maafisa wa polisi haswa kwa wale wanaaofanya biashara ya  mihadarati ambayo inadhuru afya ya watoto.

Aidha Diba amewataka machifu kushirikiana na mashirika yasiyoyakiserekali yanayopinga mila potovu kama vile ukeketaji ili kukomesha vita hivyo.

Hata hivyo afisa wa elimu katika kaunti ya Marsabit Jillo Diba,amepongeza hatua zilizopigwa na shirika la Compassion katika kuwapa elimu watoto katika kaunti ya Marsabit huku akiwataka wazazi kuhakikisha kwamba wanao wanapata elimu itakayowafaidi maishani.

Kwa upande ACC wa eneo la Marsabit Brian Mamai amewaonya wale wanaoendeleza mila potovu dhidi ya watoto kuwa watachuliwa hatua kali za kisheria.

Kadhalika Mamai amewataka wazazi kuwekeza pia katika kukuza talanta za wanao ambazo pia zinaweza kuwafaidi katika siku za usaoni.

Katika hafla hiyo wanafunzi Teresa Talaso Adano aliyepata alama 383 katika mtihani wa KCPE mwaka jana, Morola Sandei Aliyaro,Kenah Ilmogor,Ann Bare Dido,Qabale Barako Galgallo pamoja na wanafunzi wengi walituzwo zawadi mbalimbali ikiwemo begi na calculators.

Subscribe to eNewsletter