Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Grace Gumato,
Mkurugenzi wa mamlaka ya kupambana na majanga NDMA kaunti ya Marsabit, Guyo Golicha amewathahadharisha wanaMarsabit kuhusiana na hatari ya uhaba wa chakula katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.
Akizungumza na idhaa hii afisini mwake Golicha amekariri kuwa kaunti hii itaweza kushuhudia hali ya ukame ambayo itasababisha upungufu wa chakula na maji kwa binadamu na wanyama hadi mwezi wa Novemba mwaka huu.
Golicha amewataka wakulima kuhifadhi mavuno yao waliyovuna msimu uliopita ili kutoadhirika pakubwa wakati wa ukame.
Aidha Golicha amewarai wakaazi wa Marsabit ambao wanatumia mabwawa kupata maji kwa matumizi mbali mbali kuyatunza mabwawa hayo ili kujizuia na adhari zaidi wakati wa ukame.
Hata hivyo amewaonya wale ambao wanachoma nyasi katika maeneo tofauti kaunti ya Marsabit akisema kuwa ni vyema kuhifadhi nyasi kwa matumizi ya baadae.