Local Bulletins

SEREKALI YATAKIWA KUINGILIA KATI,KUTATUA MASWALA YALIYOIBULIWA NA WALIMU ILI KUZUIA MGOMO ULIORATIBIWA KUFANYIKA MWANZONI MWA MUHULA UJAO.

Na Talaso Huka na Elias Jalle,

 Serekali imetakiwa kuingilia kati na kutatua maswala yaliyoibuliwa na walimu ili kuzuia mgomo ulioratibiwa kufanyika mwanzoni mwa muhula ujao.

Kwa mujibu wa katibu mtendaji wa Chama cha walimu ya KNUT tawi la Marsabit Rose Mary Talaso ni kuwa hilo litahakikisha kwamba wanafunzi wataendelea na masomo yao kama kawaida wakati shule zitakapofunguliwa kwa muhula wa tatu mwaka huu.

Akizungumza na Radio Jangwani afisi mwake Talaso ametaja kwamba chama cha KNUT kinaunga mkono mgomo huo unaotarajiwa kuanza tarehe 26 mwezi huu wa agosti.

baadhi ya maswala ambayo walimu wanalaalmikia ni ikiwemo kukosa kuajiriwa kwa walimu wa JSS kwa mkataba wa kudumu pamoja na makubaliana ya mkataba wa maelewano CBA ambao haujatekelezwa tangu mwezi julai mwaka jana.

Subscribe to eNewsletter