Mfumo wa kutatua kesi nje ya mahakama (AJS) wazinduliwa rasmi,Marsabit.
November 23, 2024
Na Silvio Nangori
Mshukiwa wa wizi wa piki piki karibu na Shemeji inn katika eneo bunge la saku amefikishwa katika mahakama ya Marsabit.
Inadaiwa kwamba Isaak Hussein Guracha alihusika katika wizi wa piki piki aina ya Skygo yenye nambari ya usajili KMGG 787P inayogharimu Sh 241,645 tarehe 5 Juni,2023 mali ya Rob Diid Gorguro karibu na mkahawa wa Shemeji inn Marsabit Mjini.
Mbele ya hakimu Christine Wekesa, mshukiwa Isaack Hussein Guracha alikubali mashtaka dhidi yake.
Isaak alikamatwa tarehe sita Juni, 2023.
Kesi hiyo itatajwa tena hapo kesho huku akiendelea kuzuiliwa na polisi.
Wakati uo huo
Mohamed Boru Halake alifikishwa mahakamni kwa kosa la usumbufu kwa njia ya kumkosesha amani Halima Guyo halake.
Mbele ya jaji Christine Wekesa mshukiwa alikiri kosa hilo ambalo inadaiwa alitekeleza tarehe tano mwezi wa Juni katika wadi ya Sagante Jaldesa, kaunti ya Marsabit kwa kurusha mawe kwa nyumba ya Halima Guyo Halake.
Mshukiwa alikamtwa tarehe tano Juni, 2023.
Kesi yake itatatajwa tena hapo kesho.
Katika kesi nyingine ni kuwa
Galgalo Fugicha Arero alifikishwa katika mahakama ya Marsabit hii leo kwa kosa la kutishia kuzua vurugu katika mtaa wa Majengo, eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit.
Inadaiwa kuwa tarehe nne Juni, 2023 Galgallo alitishia kuharibu nyumba ya Fugicha Arero Bor Bor.
Mbele ya jaji Christine Wekesa mshukiwa alikabidhiwa dhamana ya shilingi Sh 30,000 pesa taslimu au bondi ya shilingi Sh 100,000 baada ya kukana mashtaka dhidi yake.
Kesi hiyo itatajwa tena hapo kesho tarehe nane na kusikilizwa tarehe 19 Juni.