Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Isaac Waihenya,
Waliohusika katika katika kisa cha wizi wa chakula cha msaada katika eneo la Sololo jimboni Marsabit lazima wachukuliwe hatua za kisheria.
Ndio kauli yake naibu kamishina wa kaunti ndogo ya Sololo Robert Nzuki.
Akizungunza na vyombo vya habari Nzuki amesema kwamba tayari uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na ripoti kwamba magunia 117 ya chakula cha msaada kilichopaniwa kupewa wananchi wanaoadhirika na janga la baa la njaa katika eneo hilo kilipotea kwa njia isiyoeleweka.
Nzuki amewataka wananchi kutoa taarifa kwa maafisa wa usalama zitakazofanikisha kupatikana kwa vyakula hivyo.
Kadhalika amewahakikishia wananchi kwamba chakula zaidi cha msaada kitafikishwa katika eneo hilo ili kuwasitiri wahanga wa baa la njaa.