Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Samuel Kosgei.
Kamishna wa kaunti ya Marsabit Paul Rotich ameihakikishia umma kuwa kura ya uchaguzi mkuu hapa Marsabit utafanyika kwa njia ya utulivu na Amani.
Akizungumza katika uwanja wa Marsabit wakti wa maombi kwa ajili ya jimbo, Rotich alisema kuwa wao kama serikali wameimarisha usalama na maafisa wao watazidi kushika doria ili kuhakikishia kila mwananchi usalama wake.
Wakti huo ameipa kongole baraza la dini mbalimbali hapa Marsabit kwa kile alichodai kuwa ni kujitolea kuongoza hatua za kuhubiri Amani bila kuchoka.
Aidha ametangaza kuwa tume ya uwiano na utangamano NCIC imefungua ofisi yake mjini marsabit ili kufuatilia kero la matamshi ya chuki ya kueneza uwiano.
Kwa upande wake Askofu wa kanisa katoliki jimbo la Marsabit Peter Kihara amewataka wananchi kuwachagua viongozi wanaomuogopa Mungu huku pia akiwataka watakaoshindwa kukubali matokeo ya uchaguzi bila kuzua vurugu.
Afisa kutoka tume ya uwiano na utangamano NCIC Hassan Omar amesema kuwa wanapania kuanzisha msafara wa Amani jimboni kote na kuandaliwa kwa mkutano wa mwisho wa maombi tarehe saba mwezi ujao ambapo wanasiasa wote wamelikwa.