Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Samuel Kosgei,
Mwakilishi wadi wa Kargi/SouthHorr Asunta Galgidele ameshutumu vikali ofisi ya gavana wa Marsabit kwa madai ya kukosa kuwalipa wanakandarasi ambao ndio wanaotegemewa kumalizia miradi ya maendeleo katika maeneo wadi kote jimboni.
Akizungumza na Radio jangwani Jumatano kwenye kitengo cha Taswira ya Mwanasiasa ambayo hukujia kila siku ya Jumatano jioni, Galgidele alisema kuwa wanakandarasi wanakosa kufanya kandarasi za kaunti kwa kuogopa kutolipwa licha ya wao kama MCAs kutenga pesa za kutumika kulipa wanakandarasi.
‘Tatizo ni executive, kama kaunti assembly tunafanya kazi yetu’ Alisema.
Alimtaka gavana kuwajibikia suala la miradi kutofanyika kwani kulingana naye wananchi wanaumia licha ya pesa nyingi kutengwa. Amekariri kuwa kuna mchezo mwingi katika idara ya kutoa zabuni akisema kuwa haoni sababu ya miradi kutofanywa.
Vile vile amedai kuwa mara nyingi wawakilishi wadi hawahusishwi kwenye miradi inayofaa kutekelezwa katika wadi zao hivyo kuwa ngumu kufuatilia miradi mashinani suala analotaja kama changamoto kuu.