Hali ya jua na ukavu kuzidi kushudiwa Marsabit na sehemu nyingi za nchi
January 7, 2025
By Samuel Kosgei,
Mabunge ya Kaunti wiki hii yanatarajiwa kuendeleza mjadala kuhusu BBI, wakati ambapo waakilishi wadi toka kaunti za Magharibi mwa Kenya wakidai donge nono la shilingi nusu-milioni mbali na ruzuku ya milioni 2 ya gari, kabla ya kupitisha mswada huo.
Tayari Mabunge ya Siaya, Kisumu, na Homabay yamepitisha mswada huo unaolenga kuikarabati Katiba kupitia kura ya maoni, viongozi mbali-mbali wanao-unga mkono Handsheki wakizuru maeneo tofauti tofauti kuwarai ma-MCA kutoubwaga mswada huo.
Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru na mwenzake wa Nakuru Lee Kinyanjui wamezitaka mabunge yao kuupitisha mswada huo.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu katika Wizara ya Masuala ya Ndani Karanja Kibicho, vitabu elfu-kumi vya BBI tayari vimepigwa chapa na vitasambaziwa wakenya ili waweze-kusoma na kuielewa.