Highlights

Waumini wakatoliki wahimizwa kutumia wiki takatifu kwa sala na tafakari.

NA JB Nateleng

Wakati Kanisa Katoliki linaendelea kuadhimisha Wiki Takatifu, ambayo ni kilele cha kipindi cha Kwaresma, Wakristu wamehimizwa kuitumia fursa hii kuwaombea watu wote katika jamii.

Akizungumza na idhaa hii, msimamizi wa liturjia katika Jimbo Katoliki la Marsabit, Padri Emmanuel Galgidhielle, amesema kuwa Wiki Takatifu iliyoanza na Jumapili ya Matawi ni kipindi muhimu kinachopaswa kuzingatiwa kwa uzito, kwani kinaakisi mateso, kifo na ufufuko wa Yesu Kristo ambayo ni msingi wa imani ya Kanisa Katoliki.

Padri Emmanuel amewahimiza waumini kutumia muda huu kwa tafakari ya kina kuhusu mateso ya Kristo, pamoja na kujitathmini ili kubadili mienendo yao na kuwa bora zaidi.

Aidha, ameeleza kuwa Kanisa huadhimisha fumbo kuu la imani kuanzia Alhamisi Kuu hadi Jumamosi Kuu kupitia ibada na sala maalum.

Vilevile, amesisitiza umuhimu wa Ijumaa Kuu kuwa siku ya sala na tafakari, akiwataka Wakristu kukumbuka mateso ya Yesu Kristo na kuwaombea wale wanaopitia changamoto mbalimbali katika jamii.

2 comments

comments user
https://sondakika.online

Radio Jangwani FM ni mfano bora wa jinsi vyombo vya habari vinaweza kuwa chachu ya maendeleo katika jamii. Kupitia vipindi vyao mbalimbali, wameweza kuelimisha kuhusu masuala muhimu kama afya, mazingira, elimu, na mshikamano wa kijamii. Kinachonivutia zaidi ni jinsi wanavyohakikisha kila kundi katika jamii linawakilishwa kuanzia vijana hadi wazee. Pia ubunifu wao katika kuandaa vipindi unafanya redio hii kuwa ya kipekee na yenye mvuto wa kudumu. Ni wazi kuwa nyuma ya mafanikio haya kuna timu yenye ari na kujituma. Hongereni sana Radio Jangwani FM mnaacha alama isiyofutika!

comments user
https://sondakika.online/?utm_source=google,

Radio Jangwani FM ni zaidi ya kituo cha redio ni sauti halisi ya jamii. Kupitia vipindi vyake vinavyogusa maisha ya kila siku, kituo hiki kimeweza kuleta watu pamoja, kuhamasisha mabadiliko chanya, na kutoa nafasi kwa sauti ambazo mara nyingi husahaulika. Napenda jinsi wanavyochanganya burudani na elimu, wakijadili masuala muhimu kama amani, maendeleo ya jamii, na utamaduni wetu wa kipekee. Ni wazi kwamba Radio Jangwani FM inajali wasikilizaji wake na ina dhamira ya kweli ya kujenga jamii bora. Hongereni sana kwa kazi nzuri mnayoifanya endelea kuwa mwanga kwa wengi!