Walimu 459 kutoka shule za JSS wapata mafunzo ya kidijitali kaunti ya Marsabit
Na Sabalua Moses
Zaidi ya walimu 459 kutoka shule za sekondari msingi JSS wanaendelea kupokea mafunzo ya kidijitali katika kaunti ya Marsabit
Haya ni kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa tume ya kuajiri walimu kaunti ya Marsabit Hussein Abdi akizungumza na wanahabari katika shule ya S.K.M
Hussein amesema mpango huo unapanga kuboresha masomo ya mtaala wa CBE pamoja na kusaidia walimu katika mifumo ya kidijitali katika kupata maudhui ya masomo yao na usalama wa mitandao katika mtaala wa CBE.
Mafunzo hayo yanajiri serikali kuu ikiendelea kuhakikisha kuwa mtaala wa CBE unaboreshwa nchini.
Vile vile kwa upande wake mwalimu Dennis Munene kutoka shule ya Chalbi Muslim amesema mafunzo hayo ya kidijitali itawasaidia walimu katika kupanga masomo yao na kuboresha masomo ya mtaala wa CBE.
Aidha ,kwa upande wake Clarkson Cheruyiot naibu afisa wa kidijitali ICTA mamlaka ya teknolojia ya habari na mawasiliano amesema kufikia mwisho wa mafunzo haya walimu watakuwa na uwezo wa kutumia masomo hayo ya dijitali kuboresha masomo yao shuleni.
Mafunzo hayo yamewaleta walimu kutoka kaunti ndogo ya Marsabit Central,Laisamis,Chalbi na Loyangalani



Post Comment