Highlights

Marsabit yasalia tulivu wakati wa maandamano ya kumbukumbu ya Gen-Z

Na Abdiaziz Yusuf

Huku maandamano ya kumbukumbu ya vijana wa Gen-Z yakishuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini, kaunti ya Marsabit imesalia tulivu bila usumbufu wowote.

Baadhi ya vijana waliozungumza na shajara wamesema kuwa maandamano yanapoteza muda na kuathiri shughuli za kujitafutia riziki, hasa wakati ambapo gharama ya maisha imeendelea kuwa juu.

Aidha wamesema badala ya kushiriki maandamano watawasilisha ujumbe wao kupitia sanduku la kura wakati wa uchaguzi.

Hata hivyo vijana hao wamehimizana kujitokeza kwa wingi wakati wa uchaguzi ili kuchagua viongozi wenye maono ya kuiletea nchi maendeleo bila kujali kabila au matabaka ya kijamii.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment