Serikali yaanza zoezi la kubaini jamii ndogo na zilizotengwa nchini.
Na Samuel Kosgei
Serikali, kupitia Ofisi ya Rais, imeanzisha zoezi la kubaini jamii zinazotambuliwa kuwa zilizotengwa na zenye idadi ndogo katika Kaunti ya Marsabit, kwa lengo la kuzijumuisha katika sera na mipango ya maendeleo ya serikali.
Akizungumza na Radio Jangwani baada ya kikao cha mashauriano kilichowakutanisha wawakilishi wa jamii mbalimbali za Marsabit, Kamishna wa Kaunti ya Marsabit, Stanley Kamande, amesema serikali inalenga kuhakikisha kuwa jamii zilizotengwa zinapata fursa sawa za kupata huduma za msingi, ajira na uwakilishi wa kisiasa.
Kamishna Kamande amesema serikali imejizatiti kuhakikisha kuwa hakuna jamii inayobaki nyuma katika maendeleo au kutengwa katika uundaji wa sera. Ameongeza kuwa kwa muda mrefu baadhi ya jamii zimeathiriwa na ubaguzi wa kijamii na kimaeneo, hali iliyochangia ukosefu wa usawa katika upatikanaji wa huduma na fursa za maendeleo. Jamii zinazolengwa ni zile idadi yao chini ya asilimia 0.25 kati ya idadi wakenya wote.



Post Comment