Highlights

Wakazi wa Golole wanufaika na ujenzi wa mnara wa mawasiliano

Na Nyabande Orwa

Wakazi wa eneo la Golole wadi ya Uran wanakilasababu ya kutabasamu baada ya mnara wa mawasiliano. Wakizungumza na kituo hiki wakazi hao wamesema hatua ya kuwekewa mnara huo utawasaidia katika mawasialiano na kuboresha eneo hilo kimaendeleo.

Vile vile wakazi hao wakizungumza na kituo hiki wanasema tangia Kenya kujipatia uhuru hawajakuwa na huduma za mawasiliano suala lililowatenga na maeneo mengine ya kaunti hii ya Marsabit.

Wakati uo huo wameipongeza serikali kwa juhudi za kuweka mnara huo. Vile vile wamesema sasa huduma za matibabu na elimu zitaboreka kwa wanafunzi wanaotegemea kusoma kupitia mtandao. Ni uzinduzi uliofanywa na katibu katika wizara ya kawi na nishati Kello Harsama.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment