Sport Bulletins

Ulinzi Star na Western Stima Wakabana Koo Huku Mathare United ikipata ushindi Mwembamba dhidi ya Nzoia Sugar

Picha:Hisani

By Waihenya  Isaac,

Klabu ya  Ulinzi Stars imetoka sare  ya magoli mawili na  klabu ya Western Stima Katika mechi iliyosakatwa hii leo Katika uwanja wa michezo wa Afuraha  mjini Nakuru.

Wanajeshi Ulinzi stars walikuwa wa kwanza kucheka na wavu kupitia mchezaji mkongwe Oscar Musa Wamalwa kunako dakika ya 14 katika kipindi cha kwanza, kabla ya mchezaji Barrona Oketch kuisawazishia klabu ya Western Stima kunako dakika ya 47 katika kipindi cha pili.

Kunako dakika ya 75 Kiungo Elvis Nandwa aliwapa wanajeshi uongozi kwa mara nyingine kabla ya Martin Mbaruku kufuta uongozi huo na kulazimisha vilabu hivyo kugawana alama.

Sare hiiyo  imeiacha  Klabu ya Ulinzi stars Katika nafasi ya 8 kwa alama 14 baada ya mechi 11 huku Western wakisalia Katika maeneo hatari ya kushushwa daraja – nafasi ya 17 kwa alama 7 bada ya kushiriki mechi 11.

Katika mechi nyingine iliyopigwa hii leo, Klabu ya Mathare United imeinyuka  Nzoia Sugar kwa goli moja kwa nunge ugani Kasarani.

Bao la Kipekee la vijana wa mtaani Mathare United  lilipachikwa wavuni kunako dakika ya  57 kupitia mchezaji James Kinyanjui.

Mathare sasa wanashikilia nafasi ya 16 kwa alama 8 baada ya mechi 8 huku nzuia Sugar wakiw akatika nafasi ya 12 kwa alama 11 baada ya mechi 11.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter