Sport Bulletins

Niko Tayari Kunyakua Taji La Carabao Msimu Huu – Asema Kocha Wa Spurs Jose Mourinho

Kombe La Karabao.
Picha; Hisani

By Waihenya Isaac.

Kocha Wa Klabu Ya Tottenham Hotspurs Jose Mourinho   Ametaja Kuwa Yupo Tayari Kulinyakua Taji La EFL Maarufu Kama Carabao Cup   Msimu Huu.

Mourinho Ameyataja Hayo Wakti Kikosi Chake Kinatarajiwa Kumenyana Na Brentford Hii Leo Usiku Katika Mechi Ya Nusu Faini Ya Kombe La Carabao.

Mechi Hiyo Itangaragaziwa Ugani Tottenham Hotspurs Stadium Kuanzia  Saa Tano Kasorobo.

Spurs Inalenga Kunyakua Taji Lake La Kwanza Tangu Mwaka Wa 2008 Ilipobeba Taji Hili Zama Hizo Likijulikana Kama Carling Cup Baada Ya Kuilaza Chelsea Kwa Jumla Ya Magoli Mawili Kwa Moja Ugani Wembley.

Mshindi Wa Leo Atasubiri Mshindi Kati Ya Manchester United Na Manchester City Hapo Kesho Ili Kumenyana Naye Katika Fainali Za Kombe Hilo Zilizoratibiwa Kusakatwa  Tarehe 14 Mwezi Machi Mwaka Huu  Ugani Wembley.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter