Sport Bulletins

Mariga amtaka rais wa FKF Nick Mwendwa kujiuzulu.

Nahodha wa zamani wa Harambee Stars Mcdonald Mariga wakti akiichezea timu ya Taifa.
Picha;Hisani

Na Waihenya Isaac,

Aliyekuwa nahodha wa timu ya Taifa Harambe Stars Mcdonald Mariga amekosoa kauli ya rais wa FKF Nick Mwendwa kuwa Kenya haina vipaji vya kutosha kuiwakilisha katika soka ya kimataifa.

Mchezaji huyo wa zamani wa Inter Milan ya Italia ameyataja matamshi ya Mwendwa kama matusi kwa vijana ibukia na wanaopania kuwakilisha taifa katika siku za usoni.

Mariga amemtaka Mwendwa kujiuzulu wadhifa wake maramoja na kuomba msama wadau katika sekta hiyo huku akisema kuwa kiwango cha soka katika timu ya Taifa Harambee Stars na hata ligi ya humu nchini kimedorora kwa kipindi cha miaka 7 ambayo Mwendwa amekuwa uongozini.

I’m appalled by FKF President @Nmwendwa sentiments made on live Tv that Kenya has no talented football players to compete with other nations. This is an insult & disrespect to the current ,former & all upcoming footballers who have continuously suffered playing #NickMwendwaMustGo pic.twitter.com/S4sFPsLQDd
— Mariga Macdonald (@MarigaOfficial) October 13, 2021

Mnamo siku ya Jumapili alipokuwa anahojiwa na runinga moja humu nchini baada ya timu ya Harambee Stars kupoteza goli moja kwa nunge dhidi ya Mali na kuzamisha ndoto ya kufuzu katika fainali za kombe la dunia mwaka wa 2022 nchini Qatar,Rais wa FKF Nick Mwendwa alitaja kuwa  soka ya Kenya ‘imekufa’ na hata makocha Jose Mourihno wa AS Roma au Mikel Arteta wa Arsenali hawawezi kuifufua kwani hakuna vijana walio na vipaji nchini.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter