Sport Bulletins

Cristiano Ronaldo ataka kurejea tena kwenye ligi ya Uingereza EPL

Cristiano Ronaldo akisherehekea goli katika ligi ya Italia.Picha;Hisani

Na Waihenya Isaac,

Cristiano Ronaldo anaripotiwa kutaka kukatiza hatma yake na Juventus na kuwa huru kurejea Manchester United.

Mreno huyo anakumbana na hatma finyu na miamba hao wa Italia na amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka jijini Turin.

Inaarifiw akuwa mshabuliazi  huyo anawazia kuungana tena na Mashetani Wekundu huku akiwa yuko tayari kupunguziwa mshahara wake kukamilisha hatua hiyo.

Ronaldo amesaliwa na mwaka mmoja kwenye mkataba wake na miamba wa Italia Juventus baada ya kujiunga nao akitokea Real Madrid mwaka 2018.

Licha ya hatima ya Ronaldo kuyumba, kinara wa Juve Andrea Agnelli alifichua mpango wa klabu hiyo kurefusha mkataba wa mchezaji huyo kabla ya dirisha la uhamisho kufunguliwa mwezi julai mwaka huu.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter