Sport Bulletins

Manchester United Kukutana Na Mancheser City Katika Nusu Fainali Ya Kuwania Kombe La Carabao (EFL).

Kombe la Carabao.
Picha;Hisani

By Waihenya Isaac.

Klabu Ya Manchester United United Itamenyana Na Mahasimu Wao Wa Jiji La Manchester, Mancheser City Katika Mechi Ya Nusu Fainali Ya Kuwania Kombe La EFL Maarufu Kama Carabao.

Debi Hiyo Ya Manchester Itakuwa Ya 183 Tangu Vilabu Hivyo Kubuniwa  Huku Ya Hivii Maajuzi Iliyochezwa  Desemba 12 Mwaka Huku Ikiishia Sare Ya Kutofungana Ugani Oldford.

Vijana Wa Josep Guardiola Walifuzu Katika Awamu Ya Nusu Fainali Baada Ya Kuilaza Arsenali Jumla Ya Magoli Manne Kwa Moja Huku Man United Wakifuzu Baada Ya Kuicharaza Everton Magoli Mawili Kwa Nunge.

Katika Nusu Fainali Ya Pili Brentford Ya Daraja La Kwanza CHAMPIONSHIP Itasaka Nafasi Ya Kufuzu Kwa Fainali Ya Kombe La Carabao Kwa Mara Ya Kwanza Itakapotoana Kijasho Na Tottenham Hotspurs Baada Ya  Kuilaza Newcastle Goli Moja Kwa Nunge Katika Awamu Ya Robo Fainali.

Spurs Walifuzu Baada Ya Kuikaranga Stoke City Ya Kocha Mike Oneill Kwa Jumla Ya Magoli Matatu Kwa Nunge.

Mechi Zote Mbili Zitagaragazwa Tarehe Tano Mwezi Januari Mwaka Ujao.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter