Sport Bulletins

Gor Mahia Kumenya Na  CR Belouizdad Ya Algeria  Katika Awamu  Ya Finali Ya Kufuzu Katika Awamu Ya Makundi Ya Michuano Ya Klabu Bingwa Barani Afrika CAF

Picha; Hisani

By Waihenya Isaac

Klabu Ya Gor Mahia Itamenya Na Klabu Ya CR Belouizdad Ya Algeria  Katika Awamu  Ya Finali Ya Kufuzu Katika Awamu Ya Makundi Ya Michuano Ya Kuwania Kombe La Klabu Bingwa Barani Afrika CAF Champions League.

Gor Itasafiri Hadi Jijini Algiers Kumenyatana Na Vijana Wa Frank Dumas Mnamo Tarehe 22 Mwezi Huu Kabla Ya Mechi Ya Marejeleo Kugaragazwa Wiki Mbili Baadae.

Mechi Hiyo Ya Majereleo Itapigwa Tarehe 5 Mwezi Januari Mwaka Ujao  Katika Uwanja Wa Nyayo Jijini Nairobi.

Picha; Hisani

Vijana Hao Wa Kocha Roberto Oliveira Goncalves Walifuzu Katika Awamu Hiyo  Siku Ya Jumamosi  Disemba 5 Mwaka Huu, Baada Ya Ushindi Wa Magoli 3-1  Dhidi Ya APR Ya Rwanda Na Katika  Kipute Hicho Kwa Jumla Ya Mabao 4-3.

APR Walijibwaga Uwanjani Wakijivunia Ushindi Wa 2-1 Kutokana Na Mechi Ya Mkondo Wa Kwanza Iliyochezewa Jijini Kigali Mnamo Novemba 28, 2020.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter