Highlights

Sampuli za maji zachukuliwa kufuatia vifo vya ng’ombe Korr

Na Abdiaziz Yusuf

Wasiwasi umetanda katika eneo la Korr, kaunti ndogo ya Ngurnet, kaunti ya Marsabit, baada ya ng’ombe saba kufariki dunia wakidaiwa kunywa maji kutoka kwenye kisima kilichopo eneo hilo.

Hata hivyo, chanzo halisi cha vifo hivyo bado hakijafahamika, huku uchunguzi ukiendelea.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani, mwakilishi wa wadi ya Korr, Daudi Tomasot, amesema sampuli za maji kutoka kisima hicho tayari zimechukuliwa na kupelekwa katika maabara ya serikali kwa uchunguzi ili kubaini iwapo maji hayo ndiyo yaliyosababisha vifo vya mifugo hiyo.

Tomasot amewataka wafugaji kuwa waangalifu na kusubiri matokeo ya uchunguzi kabla ya kuendelea kutumia maji kutoka kwenye kisima hicho. Ameongeza kuwa serikali itatoa taarifa rasmi mara tu matokeo ya uchunguzi yatakapokamilika.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment