Highlights

NCCK yatoa wito wa kuimarishwa kwa usalama Marsabit.

Na Nyabande Orwa

Mwenyekiti wa NCCK tawi la Marsabit, mchungaji Lole Said, ametoa wito kwa vyombo vya usalama kuimarisha ulinzi wa wananchi katika kaunti ya Marsabit.

Akizungumza baada ya viongozi wa NCCK kutembelea wafungwa katika gereza kuu la Marsabit pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha Charity Sisters mjini Marsabit, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa NCCK, mchungaji Said amesema ni jambo la kusikitisha kuwa visa vya watu kutoweka kufuatia madai ya kutekwa nyara vinaendelea kushuhudiwa nchini.

Amesema jukumu la vyombo vya usalama ni kulinda maisha na mali ya wananchi, na hivyo amevitaka kuimarisha juhudi za kuhakikisha kila raia anapata ulinzi unaostahili.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuheshimu haki za binadamu na kudumisha usalama kwa mujibu wa sheria.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment