Highlights

Marsabit yakuwa mwenyeji wa warsha ya marekebisho ya sheria za madini

Na Sabalua Moses

Wizara ya madini na uchumi wa  bahari imeandaa warsha ya kuhamasisha umma pamoja na  wachimbaji  madini katika kaunti ya Marsabit kuhusu miswada na marekebisho ya sheria katika sekta hiyo

Hafla hiyo imewaleta pamoja washikadau mbali mbali ikiwemo wachimba madini,maafisa wa serikali ya kitaifa na serikali za kaunti na wakaazi kutoka maeneo bunge ya Laisamis ,North Horr na Saku .

Akizungumza na wanahabari Franklin Mutise kiongozi wa timu hiyo kutoka wizara ya madini na uchumi wa bahari amesema miswada hiyo ina vikwazo vitatu ambavyo vina madhumuni ya kuboresha sekta hiyo ikiwemo usalama wa mazingira pamoja na rasilimali.

Kwa upande wake Francis Kamau ambaye ni mtaalam wa vilipuzi yanayotumiwa kwenye migodi amesema miswada hiyo na marekebisho yatasaidia pakubwa katika kuboresha na kuleta usalama sekta ya uchimbaji madini.

Kwa upande wake Mukhtar Golicha katibu mkuu wa wanachama  wa migodi  Marsabit amesema mapendekezo hayo ya miswada hiyo yataathiri pakubwa wachimba migodi wadogo hasa kutokana  na bei za kupata leseni.

Post Comment